Na Ester Madeghe,
Mtandao wa kijamii wa X zamani (Twitter), umesimamisha na kuifungia akaunti ya lugha ya Kiebrania ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei. Hatua hiyo imekuja saa chache baada ya akaunti hiyo kutuma ujumbe unaosema, “Utawala wa Israel ulifanya makosa. Ulikosea katika mahesabu yake kuhusu Iran. Tutaufanya uelewe nguvu, uwezo, ubinifu na ulinzi wa taifa la Iran".

Ujumbe huo wa Kamanei, unaandikwa kukiwa na mfululizo wa mashambulizi ya kigaidi ya Israel dhidi ya Iran huku utawala huo ukiendeleza vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza na Lebanon.
Mtandao wa X unaomilikiwa na Elon Musk, ambaye anaunga mkono utawala hasimu wa Israel, kitu ambacho si mara ya kwanza mashirika ya taifa la Marekani kufunga akaunti za mitandao ya kijamii zinazofungamana na Ayatullah Khamenei.
Mnamo mwezi Februari, akaunti za Facebook na Instagram za Ayatullah Khamenei ziliondolewa na Meta, kampuni ya Kimarekani inayoendesha na kumiliki mitandao hiyo mawili. Oktoba 7, 2023, Israel ilianzisha vita katika Ukanda wa Gaza, ambapo mtandao wa Meta umelenga kuondoa kila maudhui yanayoiunga mkono Palestina kwenye mitandao yake ya Instagram na Facebook.
Katika upande wa pili X (twitter) Instagram na Facebook zimejiepusha kuchukua hatua dhidi ya akaunti zozote zinazomilikiwa na maafisa wa Israel ambao wamekuwa wakichochea mauaji dhidi ya Wapalestina.
Comments