Taarifa iliyotufikia mezani inaeleza kuwa mtalii mmoja raia wa China amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea kwenye hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), imesema watalii wengine sita raia wa China wamejeruhiwa na wanaendelea kupatiwa matibabu. Shirika hili limesema bado linaendelea na uchunguzi wa ajali ya hiyo iliyohusisha gari la waongoza watalii namba T603 DCL mali ya kampuni ya Yonda Africa.
Comments