top of page

MSHAMBULIAJI WA KUJITOA MUHANGA AUWA SABA NCHINI SOMALIA

Na Ester Madeghe,


Watu saba wameuawa na wengine sita kujeruhiwa baada ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga kushambulia mgahawa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. Taarifa ya polisi imesema waathirika wa shambulizi hilo ni pamoja na maafisa na raia ambao walikuwa wakinywa chai nje ya Chuo cha Polisi cha Jenerali Kaahiye.


Kundi la wanamgambo wenye uhusiano na al-Qaeda, al-Shabab, limedai kuhusika na shambulio hilo. Shambulio hilo linakuja miezi miwili baada ya watu 37 kuuawa katika shambulio kama hilo kwenye eneo la wazi la pwani mjini Mogadishu.


Matukio haya yanaendelea kujiri wakati Somalia ikijiandaa kuchukua majukumu ya usalama kutoka kwa wanajeshi waliopo chini ya kikosi cha Umoja wa Afrika ambacho muda wao unamalizika mwezi Desemba.

コメント


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page