Na VENANCE JOHN
Mbunge wa jimbo la Kisesa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luhaga Mpina amekitaka chama chake kuwawabana mawaziri ambao sekta zao zinachangia upotevu wa mapato ya nchi.

Akizungumza katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi mkoani Simiyu, Luhaga Mpina amesema mapato mengi ya serikali ya Tanzania yanaingia mifukoni mwa watu.
Mpina amesesitiza kwamba yuko tayari kutoa taarifa ya wadhalimu wa fedha za serikali wakiwamo wanaotorosha fedha kwenda nje ya nchi ikiwa atahitajika kufanya hivyo. Katika hatua nyingine, Mpina amepongeza hatua ya rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuunda tume ya kutathimini ukusanyaji wa mapato na kodi.
Comments