Na Kulwa Mwaijulu,
Mpango huo unajadiliwa na viongozi wa nchi za Kiarabu waliokutana mjini Cairo katika mkutano wa dharura siku ya Jumanne uliobuniwa na Misri, kuwa mpango huo utawatenga Hamas katika utawala wa eneo hilo mara tu vita vitakapomalizika huku rais wa Misri akipendekeza kamati ya Palestina kutawala kwa muda Gaza.

Misri imependekeza mpango wa dola bilioni 53 wa kujenga upya Gaza kwa muda wa miaka mitano, ukilenga misaada ya dharura, urejeshaji wa miundombinu na maendeleo ya muda mrefu ya kiuchumi.
Pendekezo hilo lilikuwa likijadiliwa katika mkutano wa kilele wa Waarabu mjini Cairo siku ya Jumanne, ili kukabiliana na mpango uliotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump mwezi uliopita wa kuchukua udhibiti wa Gaza na kuwaondoa Wapalestina katika eneo hilo. Wapalestina, pamoja na mataifa ya Kiarabu na serikali nyingi duniani, wamelaani pendekezo hilo la Trump, na kukataa juhudi zozote za kuwafukuza raia wa Gaza.
Rais Abdel Fattah al-Sisi akizungumza katika mkutano huo amesema "Kwa msaada wa ndugu zangu wa Kipalestina, Misri imefanya kazi kuunda kamati ya utawala ya Palestina ya wataalamu na wanateknolojia huru, ambao watakuwa na jukumu la kutawala Gaza kwa utaalamu wa wanachama wake,".
Mpango wa hati hiyo yenye jina la "Gaza 2030" iliyo na nembo ya rais wa Misri, yenye kurasa 91 inapendekeza kuwa Misri na Jordan zifunze vikosi vya polisi vya Palestina kwa ajili ya kutumwa kulinda ukanda huo, utawasilishwa kwa Rais wa Marekani Donald Trump katika wiki kadhaa zijazo
Misri inapendekeza kuundwa kwa kamati huru ya kiteknolojia ya Palestina itakayotawala Gaza kwa muda wa miezi 6 chini ya mwavuli wa" Mamlaka ya Palestina yenye makao yake makuu katika Ukingo wa Magharibi ambayo wanachama wake hawatakuwa na uhusiano na makundi ya Wapalestina.
Comments