top of page

MOSHI WENYE SUMU INDIA WATANDA NA KUPUNGUZA MWONEKANO, SAFARI ZA NDEGE ZAHOFIWA KUATHIWA SABABU YA UCHAFUZI

Na VENANCE JOHN


Moshi wenye sumu umetanda kaskazini mwa India siku ya leo Alhamisi, na kuwa mnene kupita kiasi katika maeneo kadhaa, ikiwa ni viwango vya juu vya uchafuzi wa mazingira pamoja na unyevu, kasi ya chini ya upepo, na kushuka kwa joto.


Hata hivyo, shughuli katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa New Delhi hazikuathiriwa na moshi huo, ambao maafisa wa hali ya hewa wanatarajia kutawanyika wakati wa mchana ikiwa upepo utavuma.


Muonekano ulisalia katika mita 300, ambapo mwendeshaji wa uwanja wa ndege, Delhi International Airport Limited (DIAL) amesema, mashirika mengine ya ndege yameonya kuwa safari za ndege zinaweza kuathirika.


Kiwango cha chini cha halijoto katika jiji la Delhi kimeshuka hadi nyuzi joto 16.1 siku ya leo kutoka nyuzi joto 17 siku ya jana. Uchafuzi wake umeorodheshwa katika kategoria kali kwa siku ya pili mfululizo, ikiwa na alama 430 kwenye faharasa ya ubora wa hewa.


Jiji la Lahore katika nchi jirani ya Pakistan limeorodheshwa kuwa ndilo lililochafuliwa zaidi duniani katika janga la kila mwaka la majira ya baridi katika eneo hilo, likizidiwa na vumbi, utoaji wa hewa chafu, na moshi kutokana na moto katika majimbo ya kilimo ya India ya Punjab na Haryana.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page