Na VENANCE JOHN
Muhubiri mwenye misimamo mikali Bw. Anjem Choudary leo amehukumiwa kifungo cha maisha jela na mahakama kwa kuongoza kundi la kigaidi nchini Uingereza. Hukumu hiyo imetolewa siku chache baada ya muhubiri huyo kutiwa hatiani katika mahakama ya Woolwich Crown kwa kuwa mwanachama wa kundi lililopigwa marufuku lenye misimamo mikali la al-Muhajiroun ( ALM). Mhubiri huyo anahusishwa na kuhamasisha na kuliunga mkono kundi hilo.

Jaji Mark Wall amesema Choudary mwenye umri wa miaka 57, anaongoza kikamilifu kundi la kigaidi linalowatia moyo vijana kujiingiza katika vitendo vya misimamo mikali. Kundi la ALM lilipigwa marufuku na serikali ya Uingereza mwaka 2010 kama kundi linalojihusisha na kufanya, kupanga au kuendeleza ugaidi.
Comentarios