top of page

MCHUNGAJI ANAYEAMURU WANAWAKE KUVULIWA NGUO NA KUNYOLEWA NYWELE SEHEMU ZA SIRI ANGUNDULIKA KENYA, POLISI KUANZISHA UCHUNGUZI

Na VENANCE JOHN


Polisi nchini Kenya wamefungua uchunguzi dhidi ya mchungaji na wafuasi wa kanisa la Pentekoste katikati mwa Kenya, baada ya tuhuma za unyanyasaji wa kingono kwa wanawake kadhaa wenye umri wa kati ya miaka 17 na 70.


Kulingana na waraka wa polisi wa Kenya uliyoonwa na shirika la habari la AFP, Mchungaji Daniel Mururu aliwaamuru wazee wa kanisa na baadhi ya wasaidizi wake kuwavua nguo wanawake na wasichana, kuwanyoa nywele zao za sehemu ya siri, kunyonya matiti yao na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake na wasichana hao.


Uchunguzi huo unakuja baada ya polisi kuchunguza kisa cha kanisa kuchomwa moto katika mji wa Kianjai, ambapo chunguzi wa awali ulibaini kuwa kisa hicho kilitokana na hasira ya wakazi dhidi ya tawi la la Makanisa ya Kipentekoste ya Kenya.


Polisi wamesema wanazo taarifa za mashahidi 23 wa vitendo kama hivyo dhidi ya msichana wa miaka 17, ambaye sasa ni mjamzito. Polisi imeongeza kwa zaidi ya wanawake saba wenye umri wa miaka 17 mpaka 70 walidai kuwa waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia na kingono


Kwa mujibu wa polisi, mchungaji na wazee waliwalazimisha au kuwachochea wafuasi wa kanisa hilo kujihusisha na vitendo vichafu, wakiwaambia kuwa walikuwa katika hatari ya kuugua au kuwa tasa kama wasingefanya hivyo.


Nchi ya Kenya yenye wakristo wengi, ina maelfu ya makanisa ambapo makanisa 4,000 yanajulikana kiserikali ambapo wakati mwingine makanisa hayo huingia kwenye shughuli za uhalifu. Mwaka jana Kenya ilitikiswa na ufichuzi wa mauaji katika msitu wa Shakahola, na kugunduliwa kwa mamia ya miili ya wafuasi wa dhehebu la mwinjilisti Paul MCKenzie.

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page