top of page

MBOWE AACHIWA KWA DHAMANA, ASEMA WATAJADILI IKIWA WATAENDELEA NA MAANDAMANO

Na VENANCE JOHN


Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, Freeman Mbowe ameachiwa kwa dhamana baada ya kukamatwa kwa kile jeshi la polisi walichoeleza kuwa alikuwa anahamasisha maandamano ambayo hayakuwa na kibali.


Mbowe ameachiwa usiku wa saa tano na kusema kuwa malengo yao hayajatimia kwa kuwa hawakuandamana, hivyo baada ya kukaa kikao leo na viongozi wenzake wataamua ikiwa watandelea na maandamano. Mbowe amesema kuwa wanasheria wao waliwaagiza kutotoa maelezo yoyote polisi wakidai watatoa maelezo yao mahakamani mbele ya mahakimu au majaji wakiwa na mawakili wao.


Mbowe alikamatwa jana asubuhi maeneo ya magomeni, huku viongozi wengine wa CHADEMA wakikamatiwa maeneno tofauti tofauti. Polisi walizima maandamano hayo yaliyokuwa yameitishwa na mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, yaliyokuwa yamepangwa kufanyika jijini Dar es Salam.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page