
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu ya Mashujaa FC usiku huu inaeleza kuwa. "Uongozi wa Klabu ya Mashujaa Fc unapenda kuutarifu umma kuwa umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na kocha mkuu Mohamed Abdallah 'Baress'. Vilevile Uongozi wa Mashujaa Fc umesitisha mkataba wa kocha wa viungo Hussein Bunu pamoja na kocha wa makipa Rafael Nyendi.
Kwasasa timu itakuwa chini ya kocha msaidizi Charles Fredie wakati mchakato wa haraka wa kumpata kocha mkuu ukiendelea. Uongozi wa Klabu unapenda kuwashukuru makocha hao kwa mchango wao ndani ya Klabu yetu na unawatakia kila la kheri katika majukumu yao mapya."
Comments