Na VENANCE JOHN
Wakati utawala wa rais wa sasa wa Marekani Joe Biden ukiwa unafanya kazi ya kuharakisha uwasilishaji wa silaha kwa Ukraine katika siku zake za mwisho ofisini katika juhudi za pamoja za kuweka Ukraine kwenye msingi thabiti hadi 2025 lakini rais mteule Donald Trump amesema Biden anafanya makosa kutoa msaada wa kamombora ya ATACMS kwa taifa hilo ili kuishambulia Urusi

Msukumo huo ni tofauti kabisa na ule wa utawala wa Trump unaokuja, kwani Donald Trump amekosoa vikali hatua ya hivi majuzi ya Marekani kuruhusu Ukraine kutumia silaha zinazotolewa na Marekani kushambulia ndani ya Urusi
Trump ametoa kauli hiyo katika mahojiano na Jarida la Time lililochapisha mahojiano hayo jana Alhamisi. Katika onyesho la hivi punde la kuunga mkono Ukraine, utawala wa Biden jana Alhamisi jioni ulitangaza kifurushi cha msaada cha dola milioni 500.
Mahojiano haho na jarida la Time yalifanywa mwishoni mwa Novemba lakini yalichapishwa jana Alhamisi Trump alisema katika mahojiano hayo kwamba hakukubaliana vikali na uamuzi wa utawala wa Biden kuruhusu Ukraine kushambulia ndani ya Urusi na silaha zinazotolewa na Marekani.
"Tunazidisha vita hivi na kuifanya kuwa mbaya zaidi," Trump alisema. “Hilo halikupaswa kuruhusiwa kufanywa. Alisema Trump na kuongeza “Na nadhani hilo ni kosa kubwa sana, kosa kubwa sana.”
Comments