top of page

MANARA KANIAMBIA NIACHE KIBURI

MANARA KANIAMBIA NIACHE KIBURI

NIENDE ZNZ NIKAOMBE MSAMAHA PENGINE NITARUDIWA - DIAMOND


Baada ya Zuchu kutangaza kutemana na staa wa Bongofleva @diamondplatnumz kwenye penzi lao zito hatimaye mwamba huyo amesema anaelekea Zanzibar ambapo yupo kwa Shoo ya Full Moon Party ili aweze Kumuomba Msamaha @officialzuchu na mambo yarudi kama zamani hii ni baada ya kupigwa semina na rafiki yake Haji Manara.

"Kaka yangu @hajismanara jana alinishauri niache kiburi niende Zanzibar nikaombe Msamaha pengine nitaweza Rudiwa, Baada Kumbishia kwa Muda Mrefu nikagundua Yuko sahihi...Nami niko njiani kuelekea Zanzibar kulitekeleza hilo... Nahitaji sana mawazo yenu kwenye Ubunifu wa Kuomba Msamaha, lakini pia Uwepo wenu kwenye Full Moon Party Kendwa Rocks Zanzibar leo ili kunisaidia kulikamikisha hili kwa mlio Mikoa ya Mbali nyie msijali, nisaidieni tu kuniombea kwa kushare hii Cover, lakini pia kwa kucomment kwa ukurasa wake wa Instagram pale" - @diamondplatnumz Katika Ukurasa wake Wa Instagram.

Opmerkingen


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page