Kutoka nchini Malawi Watu wote tisa waliokuwemo katika ndege iliyombeba Makamu wa Rais

wa Malawi Dkt. Saulos Chilima wamefariki dunia baada ndege hiyo kuanguka katika msitu wa Chikangawa.
Kafuatia ajali hiyo, Rais Lazarus Chakwera wa nchi hiyo ametoa pole kwa familia za marehemu na kutangaza bendera zote nchini humo zipeperushwa nusu mlingoti mpaka marehemu watakapozikwa.
Dkt. Chilima amekuwa Makamu wa Rais wa Malawi tangu mwaka 2020.
Comments