Na VENANCE JOHN
Mahakama nchini Korea Kusini imefutilia mbali hati ya kukamatwa kwa Rais Yoon Suk-yeol aliyeondolewa madarakani mwishoni mwa mwaka jana. Hatua hiyo, inatayarisha njia ya kuachiliwa kwake kutoka jela baada ya kuzuiliwa kwa kutanganza sheria ya kijeshi kutumika ingawa ilishindwa kufanya kazi baada ya bunge la nchi hiyo kuitakaa.

Rais huyo aliwasilisha ombi hilo katika mahakama ya wilaya ya kati ya seoul mwezi uliopita, akiomba kwamba hati ya kukamatwa iliyotolewa dhidi yake ilikuwa kinyume cha sheria. "Ni jambo la busara kuhitimisha kwamba hati ya mashtaka iliwasilishwa baada ya muda wa kizuizini wa mshtakiwa kuisha," ilisema hati kutoka Mahakama ya Wilaya ya Kati ya Seoul.
Mawakili wa Yoon Suk-Yeol na ofisi yake ya rais wamekaribisha uamuzi wa mahakama, wakisema inaonyesha kesi dhidi ya Yoon ilifuatiliwa kwa madhumuni ya kisiasa bila uhalali wa kisheria.
Hata hivyo rais Yoon ambaye ni mshtakiwa ataachiliwa tu ikiwa mwendesha mashtaka ataondoa haki ya kukata rufaa, au hatawasilisha rufaa ndani ya muda uliowekwa. Chama cha upinzani cha Democratic kimekashifu uamuzi huo wa mahakama.
Comments