Mabasi mawili ya abiria moja mali ya Kampuni ya Kapricon Express na jingine la Kampuni ya Premier Line yamegongana uso kwa uso katika eneo la Sae Jijini Mbeya leo Oktoba 07, 2024.

Habari kutoka Jijini Mbeya zinasema bado taarifa za hali za watu waliokuwamo ndani ya mabasi hayo hazijatolewa na askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani na wale wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wapo katika eneo la tukio kuwaokoa watu pamoja na kuyanasua mabasi hayo.
Kwa mujibu wa mashuhuda, chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo aliyekuwa akitokea eneo la Mbeya Pazuri Social Club kuingia barabarani bila kuchukua tahadhari. Hali hiyo inadaiwa kusababisha madereva wa mabasi hayo kutafuta namna ya kulikwepa gari hilo dogo, hali iliyosababisha kugongana uso kwa uso.
Taarifa zaidi zitakujia
Comments