top of page

KWANINI MNAPENDA KUMPANGIAMTU FURAHA YAKE, KWANI KUNAMTU KAIBIWA MPENZI WAKE - SHISHI

Kutoka kwa Mjasiriamali na msanii Shilole amefunguka haya ,"Nyieeeeee Jamani hebu njooni kwanza hapa dada enu nina maongezi na nyie kidogo


Hivi Kwanini mnapenda kumpangia mtu furaha yake? Mtu akiamua kuwa na furaha na mapenzi yake na akaamua kupendana na mtu wake, hajaiba mtu wako wala hajaibiwa ameamua kuweka wazi mahusiano yake watu wanaumia wapi kwani kuna mtu kaibiwa mpenzi wake?


Alafu wanao bully watu na kupiga kelele mitandaoni ni wana wapenzi wengi hata hawajui nani wamonyeshe au hata maisha yao ya mahusiano hayana muelekeo hasira zao wanamalizia kwa watu wenye furaha na mahusiano yao. Mapenzi ni maisha, wakati ukipata nafasi ya kufurahia we furahi leo yako kesho anaijua Mungu.


Tafuteni wapenzi wenu..Kuleni mshibe mlale. Acheni roho za wivu zinawazibia rizki zenu tu Mnawapangia watu wawena kina nani, hay na nyie tuonyesheni na nyie wapenzi wenu kama mna huo ujasiri


Alafu wadada wa inbox kwa mwanaume wangu nitakuja niwanyonge mfe ovyoo. Mbona mimi siwafati wanaume zenu inbox, kujidhalilisha tu kuoga aaaah. Kesho nikiamka na vya Igunga vimepanda ntapost screenshot zenu wahalifu wakubwa msiokaa kudeal na maisha yenu.


POVU HILI LIMEMETWA KWENU KWA UDHAMINI wa HUBA LANGU NA SHEMEJI YENU. Kwani kuna Shidooo"

Comentários


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page