Klabu ya KMC imemkaribisha Nyumbani mchezaji wao Awesu Awesu baada ya taarifa hii ya Kamati ya Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) "Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake cha tarehe 10.08.2024 ilijadili shauri lililowasilishwa na klabu yako kuhusiana na usajili wa mchezaji Awesu Ali Awesu.

Malalamiko ya klabu yako ni kuwa Simba SC imemrubuni mchezaji Awesu Ali Awesu, na kumtangaza kuwa mchezaji wao katika mitandano yake ya kijamii bila kufuata utaratibu wakati suala lake likiwa bado halijatatuliwa
Kamati ilisikiliza pande zote mbili (KMC FC na Simba SC), na kuamua kuwa Awesu Ali Awesu ni mchezaji halali wa KMC FC, na kama Simba SC inamuhitaji mchezaji huyo izungumze na klabu yake.
SHIRIKISHO LA MPIRA Vilevile Kamati haikupata ushahidi wowote kutoka kwa klabu yako kuwa Simba SC ilimrubuni mchezaji Awesu Ali Awesu. Pia Kamati imetoa onyo kwa Simba SC na kusisitiza ifuate taratibu pale inapohitaji kusajili mchezaji."
Comments