Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na klabu ya Vipers ambapo taarifa hiyo ilieleza kuwa "Tuna huzuni kubwa kutangaza kifo cha ghafla na kisichotarajiwa cha mchezaji wetu mpendwa, Abubakar Lawal, ambaye alitutoka asubuhi ya leo," SC Vipers waliandika katika ujumbe mtandaoni.

Tukio lililopelekea kifo chake ni ajali iliyotokea wakati Lawal alipokuwa akielekea kwenye mazoezi ya asubuhi ya klabu baada ya kumshusha rafiki yake aliyekua amembeba kwenye pikipiki kwenye barabara ya eneo la Uwanja wa Ndege wa Entebbe.
Abubakar aliyekuwa akicheza nafasi ya kiungo mshambuliaji uwanjani ambaye pia ni raia wa Nigeria amefariki akiwa na umri wa miaka 29 akiwatumikia miamba hao wa Uganda kutoka July 2022 alipojiunga nao akitokea nchini Rwanda katika klabu ya AS Kigali.
Lawal, aliyezaliwa Septemba 3, 1995, alianza kucheza kama mshambuliaji kabla ya kuwa kama kiungo mshambuliaji, wakati akiwa Vipers SC, Lawal alicheza mechi nane katika msimu unaoendelea wa Ligi Kuu ya Uganda, ingawa hakufunga wala kutoa pasi ya bao. Mshambuliaji huyo alicheza vilabu vya Kano Pillars FC, Wikki Tourists FC, na FC Nasarawa nchini Nigeria kati ya 2014 na 2020 kabla ya ujio wake Afrika Mashariki.
Commentaires