Na VENANCE JOHN
Israeli imetangaza kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuwa mtu asiyetakiwa nchini Israel.

Nchi hiyo imempiga marufuku kuingia katika ardhi ya Israeli kwa kile ilichokieleza kuwa ni Katibu mkuu huyo kutokosoa na kulaani shambulio la Iran dhidi ya Israel. Waziri wa mambo ya kigeni wa Israeli, Israel Katz amemtaja Guterres kama mtu anayetoa msaada kwa magaidi, wabakaji na wauaji.
Hatua hiyo inakuja baada ya mataifa ya magharibi ikiwamo Marekani, Ujerumani, Uingereza na Ufaransa miongoni mwa nyinginezo kulaani shambulizi la Iran kuishambulia Israel kwa kile kilichoelezwa ni kulipiza kisasi dhidi ya Israel kwani imewauwa viongozi wa makundi ya kipiganaji inayoyaunga mkono.
Opmerkingen