top of page

KAPINGA ATOA MAAGIZO TANESCO

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga kufanya mapitio ya maeneo ya Vijiji ambayo yanalipishwa bei ya mjini kuunganisha umeme ili yaweze kulipa bei stahiki ya Vijiji ambayo ni shilingi 27,000.


Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Novemba 05, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Bukoba Vijijini, Mhe. Samsung Rweikiza aliyetaka kufahamu Serikali inachukua hatua gani kwa wananchi wa Vijijini wanaolipia gharama ya kuunganisha umeme zaidi ya 27,000.


"Kwenye baadhi ya maeneo ambayo ni Vijiji na yamekuwa yakitozwa gharama ya shilingi 321,000, , namuagiza Mkurugenzi Mtendaji TANESCO kufanya mapitio ya maeneo haya", Amesisitiza Mhe. Kapinga


Aidha, kuhusu Serikali kupeleka umeme Vitongoji visivyokuwa na umeme Bukoba Vijijini, Mhe. Kapinga amesema Serikali inaendelea kuunganisha vitongoji ambavyo havina umeme ambapo vitongoji 258 kati 515 vya Jimbo la Bukoba Vijijjini vimefikishiwa umeme.


Aidha, kazi ya kupeleka umeme katika vitongoji 27 ambavyo havina umeme katika Jimbo la Bukoba Vijijini inaendelea kupitia miradi ya ujazilizi 2B na Mradi wa Kupeleka umeme katika Vitongoji Awamu ya Pili A (HEP IIA).


Akijibu swali Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Kunti Msangi aliyetaka kufahamu Serikali inafanya jitihada gani kuondoa tatizo la umeme mdogo maeneo ya Kigamboni, Mhe. Kapinga amesema Serikali inaendelea na maboresho ya kItuo cha kupokea na kupoza umeme cha Mbagala kwa ufungaji wa transfoma yenye ukubwa wa MVA 120 ili kuimarisha upatikanaji wa umeme maeneo ya Kigamboni, Mbagala pamoja na ukanda wa Pwani.


"Transfoma imeshafika na Mkandarasi yupo site anaendelea na kazi, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Serikali ya Awamu ya Sita inafanya kila jitihada kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata umeme wa uhakika" Amesema Mhe. Kapinga

Commentaires


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page