Na VENANCE JOHN
Serikali ya Jimbo la Lagos, ambalo ni jiji la kibiashara la Nigeria limepiga marufuku matumizi ya pikipiki kibiashara katika maeneo yake yote ya jimbo hilo.

Marufuku hii inakuja baada ya kuongezeka kwa matukio ya uhalifu ikiwemo watu kuporwa mali zao na watu wanaotumia pikipiki. Jimbo hilo ambalo linaunda eneo la jiji la Lagos lina kadiliwa kuwa na jumla ya watu zaidi ya milioni 16.4 na linazalisha kipato cha Naira trilioni 41.2 sawa na dola bilioni 102 kwa mwaka.
Maeneo mengi ya majiji ya nchi za Afrika yamekuwa yakikumbwa na uhalifu wa kutumia pikipiki, hivyo kupambana na uhalifu wa aina hiyo, uongozi wa Lagos umeamua kuzuia matumizi ya pikipiki kwa shughuli zote za kibiashara, badala yake kwa matumizi ya binafsi pekee ndiyo yanaruhusiwa.
Comments