top of page

JESHI LA POLISI LAPIGA STOP MAANDAMANO YA CHADEMA

Na VENANCE JOHN


Jeshi la Polisi nchini limepiga marufu maandamano yaliyopangwa na chama kikuu cha upinzani CHADEMA. Jeshi hilo limekitaka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kusitisha mara moja mipango ya kufanya maandamano yaliyokusudiwa kufanyika Septemba 23, 2024 jijini Dar es Salaam.


Taarifa ya Jeshi hilo kupitia kwa msemaji wake David Misime linakuja ikiwa ni siku ya pili tu tangu Chadema kupitia kwa Mwenyekiti wake Freeman Mbowe kutangaza kuwa wataandamana ili kuishinikiza serikali kuwajibika kutokana na matukio ya utekaji na mauaji yaliyoripotiwa.


Misime amesema maandamano ya Chadema yanakusudia kuwatoa kwenye malengo ya uchunguzi wa tukio la kifo cha aliyekuwa kada wa chama hicho ambaye alieripotiwa kuuawa baada ya kutekwa na watu wawili wenye silaha ndani ya basi la Tashrif eneo la Tegeta akiwa safarini kutokea Dar es Salaam kwenda Tanga.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page