Na VENANCE JOHN
Wizara ya ulinzi ya Japan imesema kuwa imelazimika kuishambulia ndege ya upelelezi ya China ambayo ilivuka mpaka wa anga kwa muda mfupi na kuingia nchini humo leo Jumatatu asubuhi. Ndege hiyo ilitambuliwa kama ndege ya upelelezi ya Y-9 ambayo iliruka juu ya visiwa vya Danjo magharibi mwa kisiwa cha Kyushu kilicho Kusini kati ya saa 11:29 na 11:31 asubuhi.

Wizara hiyo imesema kuwa ni mara ya kwanza kwa ndege ya kijeshi ya China kuvuka anga na kuingia ndani ya Japan, na kwamba serikali imetoa onyo kali dhidi ya China kupitia njia za kidiplomasia.
Kando, wizara ya mambo ya nje ya Japan imesema naibu waziri wa mambo ya nje wa Japan, Masataka Okano amemwandikia barua afisa mkuu katika ubalozi wa China mjini Tokyo akimuonya dhidi ya uvamizi huo na kutaka kukoma mara moja kwa tabia hiyo.
Maafisa wa wizara ya mambo ya nje ya China hata hivyo hawakupatikana mara moja kutoa maoni yao. Hata hivyo mamlaka za Japan hazijatoa taarifa za kina kama ndege hiyo ilidunguliwa ama kuharibiwa kwa namna yoyote.
Comments