Na VENANCE JOHN
Sherehe ya chakula cha jioni cha siku ya kuzaliwa ya mwigizaji wa Hollywood Jamie Foxx ilikatizwa baada ya kutokea ugomvi katika mkahawa wa Beverly Hills, na kumwacha na jeraha, akihitaji kushonwa.

Mwakilishi wa Jamie Foxx amesembia mtu kwenye meza nyingine alirusha glasi iliyompiga mdomoni na suala hilo sasa liko mikononi mwa vyombo vya sharia. Tarrifa zinaeleza kuwa mwigizaji huyo alilazimika kushonwa na kwamba anaendelea kupata nafuu.
Haijulikani ikiwa kuna watu waliokamatwa kufuatia tukio hilo na hakuna habari nyingine iliyotolewa. Tukio hilo linakuja baada ya Foxx kufichua sababu ya kulazwa hospitalini mwezi Aprili mwaka jana.
Akizungumza wakati wa kipindi maalum cha Netflix mapema mwezi huu, mwigizaji huyo aliwaambia watazamaji kwamba alipata damu kwenye ubongo ambayo ilisababisha kiharusi. Alisema alikuwa na maumivu makali ya kichwa siku moja na akaomba aspirini, lakini kabla hajaimeza alitoka nje ndipo akapoteza fahamu na hakukumbuka chochote kwa siku 20.
Comments