Klabu ya Ihefu ambayo ilikuwa na maskani yake Mbarali mkoani Mbeya baadae kuhamishiwa Singida sasa rasmi imebadilishwa rasmi jina na sasa inaitwa Singida Black stars SC.
Maelezo ya Barua ya Ihefu ambayo kwa sasa ni Singida Black Stars, lengo la wao kubadilisha

jina ni kuwaunganisha wakazi wa Singida na timu hiyo ambapo Barua hiyo imeeleza kwamba
"Uongozi wa timu ya Ihefu Sports club iliyohamisha makazi yake kutoka Mbarali mkoani Mbeya na kwenda Mkoani Singida Umefanya mabadiliko ya jina la timu kutoka IHEFU SPORTS CLUB na sasa itatambulika kama SINGIDA BLACK STARS SPORTS CLUB
Nia na malengo ya kubadilisha jina hilo ni kuiunganisha timu na wananchi wote wa Mkoa wa Singida. Taratibu zote za usajili wa jina hilo tayari zimesha kamilika kwa kufuata miongozo, kanuni na taratibu zote za Nchi, TFF na BMT. SINGIDA BLACK STARS SC tumelenga katika kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana wa nchi yetu ili kuinua maisha yao na kutimiza ndoto zao kupitia vipaji walivyo navyo
Ni imani yetu kubwa kwambwa tutaendelea kushirikiana na wadau wote kila mmoja kwa nafasi yake kuendeleza mpira wa Nchi yetu."
Comments