Na VENANCE JOHN
Mkuu wa Jeshi la Polisi hapa nchini , IGP Camillus Wambura amesema hali ya usalama nchini ni shwari kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Jeshi la Polisi. IGP Wambura amevipongeza vyombo vya ulizi na usalama kwa kuhakikisha nchi inakuwa na amani na utulivu na wananchi wanaendelea na shughuli zao.

Pia IGP Wambura amesema jeshi la polisi limejiimarisha zaidi katika mikakati ya kuzuia uhalifu ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa kuwashughulikia wahalifu Wambura ametoa rai kwa viongozi wa dini na familia kulea jamii kwa kufuata mila, desturi na misingi ya dini ili kuwaepusha vijana kujiingiza kwenye masuala ya uhalifu.
IGP Wambura anatoa kauli hiyo huku chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA kikimtaka yeye, na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Hamad Masauni, na viongozi wengine wanaohusika na usalama wa raia kujiuzulu kufuatia taarifa zinazoripotiwa juu ya kupotea kwa watu.
Comments