top of page

HOFU YATANDA DRC WAASI WA M23 WAUTEKA UWANJA WA NDEGE WA KAVUMBA HUKO BUKAVU

Na VENANCE JOHN


Waasi wa M23 wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambao wanaungwa mkono na Rwanda wanaripotiwa kuuteka uwanja wa ndege wa kimkakati wa Kavumba karibu na Bukavu, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini.


Uwanja huo wa ndege upo takribani kilomita 20 kutoka mji wa Bukavu ambapo wakaazi wamnaeleza kuwa kuna hali ya taharuki. Msemaji wa muungano wa waasi amesema kwenye chapisho kupitia mtandao wa X, kwamba waasi wanadhibiti uwanja wa ndege na maeneo jirani.


Hatua hiyo ya waasi inakuja licha ya wito wa kimataifa wa kusitisha mapigano na kuanzishwa tena kwa mazungumzo ya amani. Maelfu ya watu wamelazimika kuyahama makazi yao katika wiki za hivi karibuni kutokana na hatua hiyo ya waasi.


Rwanda imekuwa ikikabiliwa na shhinikizo la kuwaondoa wanajeshi wake mashariki mwa Congo na kusitisha harakati za kuisaidia M23 lakini hata hivyo Rais Paul Kagame wa Rwanda anasema kipaumbele chake ni usalama.


Kagame anadai kuwa nchi yake inakabiliwa na tishio la mashambulizi kutoka kwa waasi wa Kihutu nchini Congo. Kagame pia amepuuzilia mbali tishio lolote la kuweiwekea vikwazo nchi yake. Serikali ya Kinshasa inasema Kigali inanyakua kipande kikubwa cha eneo lenye utajiri wa madini kinyume cha sheria.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page