Na Ester Madeghe,
Hezbollah ya Lebanon imeendelea kutoa vipigo katika baadhi ya maeneo ya Israel, na kuvipiga kwa makombora makali viwanda vya kijeshi vya Israel kaskazini mwa mji wa Haifa. Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, jana Jumapili, Hezbollah ya Lebanon ilitangaza kuwa, imeipiga tena kwa makombora kambi ya Zofolon yenye viwanda vya kijeshi vya Israel, kaskazini mwa mji wa Haifa.

Katika taarifa yake, kikosi cha Hezbollah kimesema kuwa, mashambulizi hayo, ni muendelezo na ishara ya kuliunga mkono taifa la Palestina huko Gaza, pamoja na kuwalinda wananchi mashujaa wa Palestina .
Mapema jana asubuhi, kikosi cha Hezbollah cha Lebanon kilifanya mashambulio na kulipiga shirika la kijeshi la Israel kusini mashariki mwa Acre, kupitia ndege zisizo na rubani. Redio ya utawala wa Kizayuni imethibitisha habari ya kushambuliwa kwa shirika hilo la kijeshi la Israel na kusema kuwa shambulio hilo limepelekea wanajeshi wasiopungua wanne wa Israel kujeruhiwa.
댓글