Kutoka kwa Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe amefunguka haya kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga SC vs Mamelodi Sundowns Jumamosi Machi 30
"Afrika inajua mechi kubwa ni moja tu ambayo ni Young Africans SC na Mamelodi. Kila mwafrika anaizungumzia mechi hii. Hii ndio mechi ambayo imetikisa zaidi AFRIKA kwa

sasa.Huu ni muda wetu, na hii ni mechi ya Muda. Hii ndio timu kubwa nchi hii. Tutavuka kwenda nusu fainali kwa soka safi"
"Hao mnaowaita wabrazil watambe wanakotambaga lakini kwenye ardhi hii hakuna wa kututambia. Tunatamba wenyewe anayebisha aseme yeye ametamba mbele yetu.....? Suala la kupandisha mnara hatutanii tunapandisha kwa yeyote"@alikamwe
"Sisi hatuna vita na Mamelodi, hatuwachukii, kama wapo wengi waje kwa wingi uwanjani. Young Africans SC lugha yetu ni amani, hatupigi wala kuzuia mtu kuja kwa Mkapa. Kama mnataka kwenda kuwapokea ndugu zenu nendeni wanafika Alhamisi. Ugomvi wetu na Mamelodi utakuwa kwenye Dakika 90 Uwanjani. Wote mnakaribishwa kwa Mkapa"@alikamwe
Comments