top of page

HATIMAYE KAMALA HARRIS AMTEUA MGOMBEA MWENZA URAIS, AMTEUA KOCHA WA ZAMANI WA MPIRA

Na VENANCE JOHN


Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democrats Kamala Harris amemchagua Tim Walz kuwa mgombea mwenza wa kiti cha urais. Tim Walz mwenye umri wa miaka 60 anatabiliwa kuwa na mbinu ya kipekee, ya kusema wazi na yenye lugha kali kwa upinzani wa Republican.


Walz pia ni mwenye wasifu wa kazi wa kuvutia na wa kipekee kwani amewahi kufanya kazi kama mwalimu wa shule ya umma, kocha wa mpira wa miguu na Mlinzi wa Kitaifa kabla ya kuingia kwenye siasa.


Uzoefu wake wa kisiasa, akiwakilisha wilaya inayoegemea chama cha Republican katika Bunge la Congress na kisha kupitisha sera za mrengo wa kushoto kama gavana wa Minnesota, inaweza kuwa na mvuto mpana wakati siasa za Marekani zikiwa na mgawanyiko mkubwa.


Bw. Walz alizaliwa kijijini Nebraska, alikuwa mkulima na mwindaji wakati wa kiangazi na alijiunga na Jeshi la Walinzi wa Kitaifa akiwa na umri wa miaka 17. Alihudumu katika kikosi cha kujitolea kwa miaka 24.Baba yake Walz alikuwa msimamizi wa shule ya umma, alimhimiza Walz kujiunga na jeshi kabla ya kufariki kutokana na saratani ya mapafu wakati Bw Walz alipokuwa na umri wa miaka 19.


Akiwa na shahada ya ualimu, Bw Walz alichukua kazi ya kufundisha kwa mwaka mmoja nchini China wakati wa mauaji ya Tiananmen Square. Baadaye alikwenda fungate nchini humo na mke wake Gwen Whipple na pia alipanga safari za kipindi cha kiangazi za elimu nchini China kwa wanafunzi wa Marekani.


Baada ya kurejea nyumbani Nebraska, Bw Walz alikuwa mwalimu na mkufunzi wa kandanda wa Marekani hadi mkewe ambaye ni mwalimu katika shule akamvuta na kumrudisha Minnesota alikozaliwa kisha kuoana. Sasa wana watoto wawili.


Bw. Walz alifanya kampeni kama mtu mwenye msimamo wa wastani ambaye alijali utumishi wa umma na utetezi wa maveterani, na hivyo kusababisha kuungwa mkono hali iliyompa ushindi na kuwa gavana wa Minnesota.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page