Na VENANCE JOHN
Jeshi la Israeli limesema moja ya miili minne ya mateka iliyorejeshwa kutoka Gaza kwenda Israeli hapo jana Alhamisi si wa Shiri Bibas, ambaye ni mmoja wa mateka kama ilivyodaiwa na Hamas,.

Shiri Bibas, mwenye umri wa miaka 33, ambaye alikuwa mama wa watoto wawili ambao ni wawili, Ariel na Kfir, ambao sasa wangekuwa na umri wa miaka mitano na miwili, vifo vyao vilisababisha maombolezo makubwa nchini Israeli.
Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF) limeitarifu familia ya Bibas kwamba miili ya watoto wake imetambulika baada ya mabaki yao kukabidhiwa na Hamas hapo jana lakini mwili wa tatu haukuwa wa mama yao
Kufikia sasa, Hamas bado haijatoa maelezo kuhusu dai la Israeli kuwa mwili huo sio wa mama wa watoto hao wawili. Utambuzi huo unajiri baada ya Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel kukabidhiwa miili minne ya mateka na kuwapeleka kwenye taasisi ya uchunguzi ya Abu Kabir huko Jaffa kwa ajili ya utambuzi rasmi.
Comments