Na VENACE JOHN
Hamas itakabidhi miili ya mateka siku ya leo akiwamo ya mtoto mchanga wa Kiisraeli Kfir Bibas na kaka yake Ariel mwenye umri wa miaka minne. Mateka hao wawili wachanga zaidi walichukuliwa na Hamas katika shambulio lao la Oktoba 7, 2023 na kuacha alama yenye kiwewe zaidi juu ya kilichotokea siku hiyo.

Magari ya shirika la Msalaba Mwekundu yaliondoka kwenye eneo la makabidhiano katika Ukanda wa Gaza yakiwa na majeneza manne meusi. Kila moja ya sanduku lilikuwa na picha ndogo ya mateka.
Hamas imekabidhi miili ya wavulana hao wawili na mama yao Shiri Bibas, pamoja na ile ya mateka wa nne, Oded Lifschitz, chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza yaliyofikiwa mwezi uliopita kwa kuungwa mkono na Marekani na upatanishi wa Qatar na Misri.
Mamia ya watu wamekusanyika kwenye baridi kali kabla ya makabidhiano hayo huko Khan Younis kusini mwa Gaza. Wanamgambo wa Hamas wenye silaha waliovalia sare nyeusi wakitanda eneo hilo. Mpaka sasa mateka 19 wa Israel wameachiliwa huru, pamoja na raia watano wa Thailand ambao walirejeshwa katika makabidhiano.
Comentarios