Na Ester Madeghe,
Mwanajeshi wa Israel aliyekuwa ameshikiliwa na jeshi la Hams, ameviambia vyombo vya habari kwamba Hamas imemruhusu yeye na wafungwa wengine kwenda kusherehekea mila na sikukuu za Kiyahudi, na kuwaruhusu kutekeleza mila zao za kidini.

Mwanajeshi huyo wa Israel anasema kwamba yeye na mateka wengine "walishangazwa" wakati Hamas ilipowapatia vitu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vitabu vya maombi vya Kiyahudi, vinavyojulikana kwa Kiebrania kama siddur.
"Hatujui jinsi ilivyokuwa, lakini walitukabidhi tu vitabu vya maombi," na kuongeza kuwa, suala hilo kwake "lisilo la kawaida."
Comments