Hatimaye klabu ya Real Madrid ya Hispania imetangaza rasmi kuwa imefikia makubaliano ya kumsajili Kylian Mbappe kwa mkataba wa miaka mitano ambapo post ya kutangaza taarifa

hizo kwenye mtandao wa Instagram imepata Likes ndani ya Dakika 30.
Aidha tovuti (Website) ya Real Madrid imezidiwa kiasi kwamba imeshindwa kuhimili kiasi cha watu duniani wanaofuatilia taarifa hiyo.
Mbappe anajiunga na Real Madrid baada ya kucheza PSG kwa miaka 7 toka pale alipojiunga nao 2018 akitokea Monaco kwa uhamisho wa euro milioni 180 ambapo hadi anaondoka Mbappe aliifungia PSG magoli 162 katika Ligi Kuu ya Ufaransa na kutwaa mataji sita.
Comentarios