top of page

Cristiano Ronaldo Kukosa Mchezo Wa Hatua Ya 16 Ligi Ya Mabingwa Barani Asia

Na Kulwa Mwaijulu,


Mshambuliaji wa Klabu ya Al Nassr Cristiano Ronaldo anatarajiwa kuukosa mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya 16 ligi ya mabingwa barani Asia kutokana na jeraha dogo.


Akiongea na waandishi wa habari kocha wa klabu hiyo Stefano Pioli amesema kuwa Ronaldo alikuwa na tatizo la kimwili hivyo hatokua sehemu ya mchezo unaotarajiwa kupigwa leo ambapo Al Nassr watakua wageni wa klabu ya Esteghlal ya nchini Qatar.


Mpaka sasa Ronaldo mwenye umri wa miaka 40 amefunga mabao 25 katika mashindano yote akiwa na Al-Nassr msimu huu wakati klabu yake ikiwa katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Saudi Arabia.

Comentários


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page