top of page

CONGO DRC YAPIGA STOP NDEGE ZOTE ZA RWANDA KUTUMIA ANGA YA CONGO DRC

Na VENANCE JOHN


Kutokana na mzozo unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, serikali ya Kinshasa imepiga marufuku ndege zote zilizosajiliwa nchini Rwanda kutumia anga yake. Serikali ya Kongo imechukua uamuzi huo jana Jumanne na kueleza kuwa ndege zote za kiraia na za serikali zilizosajiliwa Rwanda au kwingineko lakini zenye makao yake nchini Rwanda sasa ni marufuku kuruka juu ya anga ya DRC.


Hatua hii ni kutokana na vita vya kichokozi vilivyosababisha vifo vya watu 3,000 huko Goma baada ya muungano wa waasi likiwemo kundi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda kufanya uhalifu huo.


Wataalamu na wachambuzi wanasema hatua hii itakuwa pigo kwa Rwanda kutokana na ukubwa wa anga ya Kongo, lakini wanahoji ni namna gani serikali ya Kinshasa itaweza kutekeleza hatua hiyo.


Hasa ikizingatiwa kuwa mwishoni mwa mwaka 2024, taarifa za Umoja wa Mataifa zilieleza kuwa Rwanda ilivuruga mawasiliano ya anga huko mashariki mwa Kongo , jambo lililohatarisha maisha ya abiria waliopanda ndege za kibiashara eneo hilo.

Kommentare


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page