Na Ester Madeghe,
Mashindano ya kwanza ya riadha ya roboti yenye muundo wa mbwa ambayo pia ni mashindano ya roboti ya dunia ya Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) yamefanyika hapo jana Alhamisi.

Mkuu wa CMG Shen Haixiong amesema, mashindano hayo yanayofanyika kupitia CMG ambalo ni jukwaa la vyombo vya habari, yataonesha mafanikio ya uvumbuzi mpya wa roboti.
Haixiong amesema anatumaini kuwa mashindano hayo yatahimiza uboreshaji wa teknolojia ya roboti, na kuchangia ujenzi wa nchi yenye nguvu ya sayansi na teknolojia, na ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
Comments