top of page

CHINA YALAANI MATAIFA YANAYOKIUKA MAMLAKA ZA MATAIFA YA ASIA MAGHARIBI

Na Ester Madeghe,


Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya China Lin Jian, amesema kuwa, Beijing inapinga vikali hatua ya kukiukwa mamlaka ya kitaifa na mataifa mengine.


Lin Jian amesema hayo akijibu hatua ya hivi karibuni ya kichokozi ya utawala wa Israel dhidi ya Iran na kusisitiza kwamba, China inapinga hatua yoyote ya kukiuka mamlaka ya kitaifa na usalama wa nchi nyingine wa kutumia nguvu na mabavu.


Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya China ameongeza kuwa, hali ya sasa katika Asia Magharibi ni ya wasiwasi sana na wahusika wanapaswa kujiepusha kuongeza hatari za usalama katika eneo hilo.


Kadhalika, vile vile amesema, baadhi ya matukio kwa mara nyingine tena yameonyesha udharura na ulazima wa kusitishwa mapigano na kuhitimisha vita. Jumuiya ya Kimataifa, hasa madola yenye ushawishi, yanapaswa kuwa na jukumu la kujenga na kuchukua hatua muhimu katika kupunguza mivutano ya kikanda.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page