top of page

CHAMA TAWALA NCHINI BOTSWANA CHASHINDWA UCHAGUZI BAADA YA MIAKA 58, MATOKEO YA AWALI YANAONYESHA

Na VENANCE JOHN


Chama tawala cha Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi cha Botswana Democratic Party (BDP) kimepoteza wingi wa wabunge katika uchaguzi uliofanyika hvi karibuni matokeo haya yakiwa ya mshtuko kwani haikutarajiwa.


Botswana Democratic Party (BDP), ni chama ambacho kimetawala taifa hilo lenye utajiri wa madini ya almasi Kusini mwa Afrika tangu mwaka 1966. Hesabu zilizotolewa na tume ya uchaguzi zinaonesha kwamba vyama vya upinzani vimepata angalau viti 35 kati ya 61 bungeni.


Chama cha Umbrella for Democratic Change, kinachoongozwa na wakili wa haki za binadamu aliyesoma chuo kikuu cha Harvard, Bw. Duma Boko, kimeshinda viti 22 na Chama cha Botswana Congress, kinachoongozwa na mwanauchumi Bw. Dumelang Saleshando, kimepata viti 8. Nacho chama cha Botswana Patriotic Front, kilichoanzishwa na wafuasi wa Rais wa zamani Bw. Ian Khama baada ya kuondoka kutoka BDP, kimepata viti vitano.


Mpaka kufikia leo saa 05:04 alfajiri, tarehe 1 Novemba 2024, vyama vya upinzani vimepata zaidi ya nusu ya viti vya ubunge hii ikimaanisha kuwa sasa chama cha Botswana Democratic Party (BDP) kimepoteza rasmi mamlaka ya serikali. Chini ya katiba ya Botswana, chama ambacho kinashikilia viti vingi vya ubunge kinaweza kuchagua rais na kuunda serikali.


Vyama vya upinzani vimepata zaidi ya nusu ya viti vya ubunge. Hii ina maana kwamba chama tawala cha Botswana Democratic Party (BDP) sasa kimeshindwa rasmi katika uchaguzi huo. Masisi, mwenye umri wa miaka 63, mwalimu wa zamani wa shule ya upili na mfanyakazi wa UNICEF, alikuwa anatarajiwa sana kushika wingi wa wabunge na kuhudumu muhula wa pili na wa mwisho.


Kabla ya upigaji kura, chama cha BDP kilikubali hitaji la kubadilisha uchumi, na kuahidi kuendeleza vichocheo vipya vya ukuaji kama vile kilimo na utalii ingawa changamoto kubwa ilikuwa ni ukosefu wa ajira kuongezeka hadi asilimia 27, na sehemu kubwa zaidi ya vijana wasio na kazi.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page