top of page

BONI YAI MEYA WA ZAMANI KUENDELEA KUSOTA RUMANDE, MAHAKAMA KUAMUA OKTOBA MOSI

Na VENANCE JOHN


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya kada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Boniface Jacob maarufu kama Boni Yai mpaka Tarehe 1 Oktoba 2024, kwa ajili ya kutolewa maamuzi mawili.


Maamuzi ya kwanza yanayotajiwa kufanywa ni kuhusu dhamana yake, huku maamuzi ya pili yakiwa ni kiapo cha ziada kilichowasilishwa leo na upande wa mashtaka, ambapo kimepingwa vikali na wakili wake Peter Kibatala, wakili anayemuakilisha Boniface Jacob kwenye shauri hilo.


Leo tarehe 26 Septemba 2024, Mahakama ilitarajiwa kuja kwa ajili ya kutoa uamuzi kuhusu dhamana ya Boniface Jacob, lakini upande wa mawakili wa serikali walikuja na kiapo kingine kipya ambacho walihitaji kiwe sehemu ya shauri hilo licha ya kupingwa na upande wa pili.


Hakimu mkazi mfawidhi Franco Kiswagwa, alisikiliza hoja za pande zote mbili, kuhusu kiapo hicho na kuelekeza kuwa Mahakama itatoa maamuzi ya maombi hayo mawili tarehe 1 Oktoba 2024.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page