top of page

BINTI WA JACOB ZUMA KUOLEWA NA MFALME WA ESWATINI MWENYE WAKE 11 MAANDALIZI YAPO SAFI

Na VENANCE JOHN


Binti wa rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma anatarajia kuolewa na mfalme wa Eswatini. Binti huyo kwa sasa ana umri wa miaka 21 na ataolewa na mfalme wa Eswatini ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 56.


Uchumba wa Nomcebo Zuma na Mfalme Mswati wa Tatu wa Eswatini ulifanyika rasmi ndani ya wiki hii mwishoni mwa sherehe ya siku nane sherehe ambayo ni ya kitamaduni ya wasichana inayofanyika kila mwaka. Mfalme Mswati yupo katika ndoa ya mitala na wanawake 11 na ameoa mara 15 kwa jumla, hivyo binti wa Zuma atakuwa mke wa 12.


Wakosoaji nchini Eswatini wanamtuhumu mfalme Mswati, ambaye anatawala kwa amri na amekuwa kwenye kiti cha ufalme kwa miaka 38, akiishi maisha ya anasa na wanawake zake huku wengi wa wananchi wake wakitaabika katika umaskini. Eswatini, ambayo hapo awali ilijulikana kama Swaziland, ina wakazi milioni 1.1 na ni nchi moja wapo yenye viwango vya juu zaidi vya maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU).

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page