top of page

BILIONEA WA MIAKA 91 AFARIKI MIEZI 2 BAADA YA KUOA MKE WA SITA MWENYE MIAKA 42

Tajiri mhandisi kutokea Austria, Richard Lugner amefariki dunia Agosti 12, ambapo alipatikana nyumbani kwake huko Vienna akiwa amefariki. Inaaminika kuwa alikuwa akishughulikiwa na masuala mengi ya kiafya kabla ya kifo chake na alikuwa amefanyiwa upasuaji miezi kadhaa iliyopita.





Imeripotiwa kuwa tajiri huyo alikuwa amefunga pingu za maisha kwa mara ya sita katika miezi michache iliyopita kabla kifo chake. Lugner alifunga ndoa na Simone Reiländer, 42, kwenye Ukumbi wa Jiji la Vienna mnamo Juni 1.


Marehemu Lugner, alizaliwa Vienna mnamo 1932, alikuwa mwenye kufaulu masomo yake vyema na kufanikiwa kuhitimu kwenye Chuo cha Ufundi na Biashara cha Shirikisho, ambapo alibobea katika ujenzi wa majengo. Alianza kazi yake ya kufanya kazi katika kampuni ya ujenzi kwenye mji mkuu wa Austria kabla ya kupata leseni yake kama mkandarasi wa ujenzi na kuunda biashara yake mwenyewe.


Kampuni ya Lugner iliendelea kuwa maarufu kwa kujenga msikiti wa kwanza wa Vienna na baadaye Stadttempel, akajenga sinagogi kuu la jiji hilo. Marehemu mwenye umri wa miaka 91 aliendelea kujenga duka kubwa (Mall ) lenye maduka mengi makubwa ndani yake lililoitwa Lugner City, kitu ambacho kilikuja kuwa sehemu kubwa ya urithi wake.


Lilipofunguliwa jengo hilo mnamo 1990, Lugner alimwalika mwimbaji wa Marekani, Harry Belafonte kwenye duka hilo na Kuanzia wakati huo aliendelea kualika watu mashuhuri kila mwaka kuja kutembelea Lugner City na kisha kuwachukua kama wageni wake. Baadhi ya watu mashuhuri ambao walialikwa Vienna kwa miaka mingi ni pamoja na Goldie Hawn, Kim Kardashian na Kris Jenner, Raquel Welch, Jane Fonda na Priscilla Presley.


Heshima za mwisho zimekuwa zikitolewa kwa Lugner baada ya kifo chake, huku kituo cha ununuzi cha Lugner City kikiongoza machapisho kwenye mitandao yake ya kijamii. "Mhandisi wetu Richard Lugner na zaidi ya yote boss wetu mpendwa ametuacha leo," chapisho lililoshirikiwa kwenye Facebook siku ya jana linasomeka hivi ,"Hatuwezi kuweka kwa maneno maumivu tunayohisi.


Huzuni ni kubwa sana, lakini tunataka kutafakari juu ya nyakati zote nzuri na kubwa pamoja. Kwa kucheka na jicho la majonzi tunasema kwaheri kwa Richard Lugner mkuu, katika mioyo yetu atakaa milele!" Kansela wa nchi hiyo, Karl Nehammer, pia aliandika kwenye X, "Richard Lugner alikuwa mjasiriamali aliyefanikiwa na mtu wa kuvutia. Jasili wa Austria ambaye hakuwahi kupotea njia. Apumzike kwa amani!" Marehemu ameacha watoto wanne ambao ni Jacqueline, Nadine, Alexander, na Andreas.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page