
Kutoka mkoani Morogoro Asha Hassani mkazi wa Mawenzi mkoani humo anayedaiwa kuwa ni mwanachama wa Simba, amefariki dunia huku ikielezwa kuwa tatizo lilianzia wakati akifuatilia mechi ya NBC Premier League kati ya Yanga SC dhidi ya Tabora United iliyochezwa Novemba 7, 2024.
Kaka wa marehemu na majirani waelezea namna mnazi huyo wa soka alivyofikwa na umauti ambapo wamesema alipata presha wakati mchezo ukiendelea ambapo alikimbizwa hospitali ambapo baadae alifariki wakati huduma za matibabu zikiendelea.
Comments