top of page

Argentina yatangaza maombolezo ya siku tatu baada ya mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya watu 16

Na Kulwa Mwaijulu


Argentina imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia mafuriko yaliyogharimu maisha ya watu 16 huko Bahia Blanca, ambapo mvua ya kubwa ilinyesha ndani ya masaa machache, na kusababisha vitongoji kadhaa kusombwa na maji.


Rais wa nchi hiyo Javier Milei ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa Jumapili jioni baada ya mamlaka kuongeza idadi ya vifo hadi kufikia watu 16 waliopoteza maisha na wengine idadi kubwa bado hawajulikani walipo.


Mafuriko hayo mabaya yalitokea Ijumaa wakati mvua kubwa iliponyesha katika muda wa saa chache karibu na Bahia Blanca, mji mkubwa wa bandari ulioko kusini mwa mkoa wa Buenos Aires, huku vitongoji vyote vikiwa vimefunikwa na maji yanayoongezeka kwa kasi.


Wapiga mbizi wamekuwa wakiendelea kupekua katika katika maeneo na vijiji ambavyo vimekumbwa na mkasa huo ambapo bado maeneo mengi hayajafikiwa na waokoaji hao huku ikielezwa uwepo wa changamotto ya vifaa vya uokoaji.


Meya wa Bahia Blanca Federico Susbielles, wakati huo huo, aliuambia mkutano na waandishi wa habari kwamba mafuriko hayo yamesababisha uharibifu wa miundombinu ya dola milioni 400.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page