
Aliyekuwa kocha wa timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars), Adel Amrouche ametangazwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya soka ya Rwanda maarufu kama 'Amavubi'.
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Rwanda (FERWAFA) imebainisha kuwa Amrouche atakuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya soka huku kocha msaidizi namba moja akiwa Eric Nshimiyimana na Carolin Braun akiwa kocha msaidizi namba mbili.
Comments