Na VENANCE JOHN
Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini Mwanza imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Yahya Nawanda katika kesi ya kulawiti iliyokuwa ikimkabili. Uamuzi huo ulikuwa wa kesi ya jinai namba 1883/2024, yenye kosa la kulawiti, na uliosomwa na hakimu, mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Erick Marley.

Katika uamuzi huo, hakimu Marley amesema mahakama hiyo baada ya kupitia maelezo ya ushahidi na vielelezo imejiridhisha kuwa hakukuwa na muunganiko wa ushahidi unaoweza kumtia mshtakiwa Dk. Nawanda hatiani na hivyo kumwachia huru.
Comments