top of page

ALIKO DANGOTE APITWA UTAJIRI NA BILIONEA WA AFRIKA KUSINI

Na VENANCE JOHN


Bilionea wa Afrika Kusini Johann Rupert amempiku mfanyabiashara wa viwanda kutoka Nigeria Aliko Dangote kama mtu tajiri zaidi barani Afrika. Hii ni kulingana na takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na jarida la faharasi ya mamilionea (Bloomberg Billionaires Index).


Bw Rupert anadhibiti kampuni ya Richemont, ambayo ni mojawapo kampuni kubwa zaidi ya bidhaa za anasa/starehe duniani, ambayo inamiliki chapa kama vile Cartier na Montblanc. Thamani yake imepanda kwa $1.9 bn hadi $14.3bn, na kumfanya kuwa katika nafasi ya 147 duniani, nafasi 12 mbele ya Bw Dangote.


Utajiri wa bwana Dangote umepungua kwa $1.7 bilioni mwaka huu, na kufikia $13.4 bilioni. Kushuka kwa utajiri wa Bw Dangote kunadhihirisha mazingira magumu ya kiuchumi ya nchini Nigeria, ambapo kampuni nyingi zake zinafanya shughuli.


Kuporomoka kwa kasi kwa thamani ya sarafu ya naira kumemuathiri pakubwa Bw Dangote, ambaye utajiri wake unahusishwa kwa kiasi kikubwa na mali zinazotumiwa katika sarafu ya nchi hiyo.


Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page