top of page

AJALI YA TRENI YA ABIRIA

Taarifa iliyotufikia mezani hivi punde inaeleza kuwa


"Shirika la Reli Tanzania TRC linautaarifu umma kuwa treni ya abiria namba Y14 ikiwa na kichwa cha treni namba 9002, mabehewa 12 ya abiria, behewa moja la vifurushi (parcel) na behewa moja la breki imepata ajali kati ya Stesheni ya Kazuramimba na Uvinza mkoani Kigoma majira ya Saa 7:30 usiku tarehe 28 Agosti 2024.


Ajali imetokea baada ya mabehewa sita (6) ya treni kuacha njia na kupelekea majeruhi 70, wanawake 26 na wanaume 44. Treni ilikuwa na jumla ya abiria 571 wakisafiri kutoka Kigoma kuelekea mikoa ya Tabora, Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.


TRC kwa kushirikiana na Kitengo cha Afya cha Mkoa wa Kigoma walifanikiwa kuwapeleka majeruhi katika hospitali ya Wilaya ya Uvinza kwaajili ya matibabu. Hali za afya za abiria zinaendelea kuimarika, majeruhi 57 tayari wameruhusiwa, nane ( wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Uvinza na watano (5) wamehamishiwa Hospitali ya Maweni kwaajili ya matibabu. Treni iliendelea na safari kuelekea mikoa ya Tabora, Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam.


Shirika linawapa pole majeruhi na linaendelea na jitihada za kuwahudumia. Hakuna taarifa ya vifo vilivyotokana na ajali, taarifa zaidi zitaendelea kutolewa."

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page