top of page

25 WAFARIKI KATIKA AJALI YA BOTI VISIWANI COMORO

Na Ester Madeghe,


Takribani watu 25 wamefariki dunia kwenye visiwa vya Comoro baada ya kupinduka kwa mashua waliyokuwa wamepanda, shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limethibitisha tukio hilo.


"IOM Comoro ina huzuni kusikia kuhusu vifo vya watu wasiopungua 25 baada ya boti yao kupinduliwa kimakusudi na wasafirishaji kutoka Visiwa vya Comoro, kati ya Anjouan na Mayotte Ijumaa usiku," IOM ilisema katika taarifa yake.


IOM, ikiwanukuu walionusurika, ilisema mashua hiyo ilikuwa imebeba takribani watu 30 kutoka mataifa tofauti, miongoni mwao wakiwa wanawake saba na watoto wanne. "Manusura watano waliokolewa na wavuvi Jumamosi asubuhi," IOM imesema.


Mnamo Septemba, mashua iliyokuwa na watu 12 iliyokuwa ikisafiri kutoka Anjouan ilishindwa kufika Mayotte, wakati mwezi Agosti watu wanane walikufa katika tukio kama hilo, na kuongeza kuwa maelfu wamekufa kwenye njia hii tangu 2011 walipokuwa wakijaribu kufika Mayotte.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page